Thursday, July 12, 2012

Yanga yatangaza jeshi lake la Kagame

 ZIKIWA zimesalia siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Kagame kuanza, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji, Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaocheza huku akimtema nahodha wake, Shadrack Nsajigwa .


Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi, keshokutwa Jumamosi na siku hiyo itafungua kwa kuanza kucheza na Atletico ya Burundi.


Akitangaza kikosi hicho, Tom alisema haikuwa kazi rahisi kwake kupata kikosi hicho kutokana na viwango vya wachezaji wake kwenye tim hiyo.


Saintdiet alisema, wachezaji ambao amewaacha wasisikitike akiwemo Nsajigwa anatambua umuhimu kwenye timu na badala yake waendelee na mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mbelgiji huyo amekitaja kikosi hicho kuwa ni makipa ni Yaw Berko na Ally Mustapha ‘Bartherz’, Mabeki ni Juma Abdul, Godfrey Taita, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani ‘Vidic’, Ladislaus Mbogo.


Viungo ni Athumani Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Rashidi Gumbo, Nizar Khalfani, Shamte Ally na Idrisa Rashidi


Washambuliaji ni Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Said Bahanuzi na wachezaji aliowaacha ni Stephene Mwasyika, Ibrahim Job, Said Mohamed, Nsajigwa.


Wengine walio achwa ni Omega Seme, Frank Domayo na Simon Msuva waliopo Timu ya taifa ya vijana ya U-20, Nurdin Bakari mwenye majeraha ya paja.

No comments:

Post a Comment