Monday, August 13, 2012

IVANOVIC ALIPEWA KADI NYEKUNDU HEWA, KUTOFUNGIWA HATA MECHI MOJA

Seeing red: Ivanovic is sent off by Kevin Friend 
Ivanovic akitolewa nje na Kevin Friend
Flashpoint: Kolarov is floored by Ivanovic   
Kolarov akiangushwa chini na Ivanovic


BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic hatapewa adhabu yoyote ya kukosa mechi licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu jana katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyofungwa na Man City.
Mserbia huyo alitolewa nje mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu mwananchi mwenzake, Aleksandar Kolarov na refa Kevin Friend akamlimla nyekudu ya papo kwa papo.
Iliripotiwa kwamba Ivanovic atafungiwa mechi tatu, kuanzia mechi ya ufunguzi ya Chelsea ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Wigan Jumapili ijayo, pamoja na hayo mabadiliko ya sheria za FA Agosti mwaka 2009, yanayosema kadi nyekundu katika mechi za kujiandaa na msimu mpya haitamzuia mchezaji kucheza mechi za mashindano ndio yanamnusuru.
Kwa mabadiliko hayo ya sheria yanayohusu mechi zote zisizo za mashindano za kujiandaa na msimu mpya, ikiwemo mechi ya Community Shield, inamaanisha Ivanovic atakuwa huru kucheza Uwanja wa DW

Kolarov akiangushwa chini na Ivanovic

No comments:

Post a Comment