Na Princess Asia, Cairo
TOUT Puissant Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imejiweka sawa kwenye mbio za
kuwania ubingwa wa Afrika, baada ya kuifunga
Zamalek ya Misri nyumbani kwao, Cairo mabao 2-1.
Shukrani kwake,
mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’
aliyefunga bao la ushindi katika mchezo uliomalizika dakika chache zilizopita
kwenye Uwanja wa chuo cha Jeshi, Al-Qahirah mjini Cairo, dakika ya 44,
akiunganisha pasi ya Tressor Mputu Mabi.
Katika mchezo huo wa
Kundi B, Himoonde alitangulia kuifungia Mazembe inayofundishwa na Lamine
N'Diaye dakika ya 34 pasi ya Mputu, lakini Omotoyossi akaisawazishia Zamalek
inayofundishwa na kocha Jorvan Vieira dakika ya 36, pasi ya Mohamed Ibrahim.
Ushindi huo wa kwanza
ugenini kwa Mazembe katika hatua ya makundi, unaifanya Mazembe ifikishe pointi
saba, baada ya kucheza mechi nne, kushinda mbili, sare moja na Berekum Chelsea
na kufungwa moja na Al Ahly ugenini.
Al Ahly iliyotoa sare
ya 1-1 na Berekum Chelsea nchini Ghana leo, bado inaongoza kundi hilo kwa
pointi zake 10, wakati wababe wapya wa Ghana wanashika nafasi ya tatu kwa
pointi zao tano na Zamalek wanashika mkia wakiwa hawana pointi hata moja.
Kwa mara ya kwanza,
katika mchezo wa leo, mshambuliaji mwingine wa Tanzania, Thomas Emmanuel
Ulimwengu alikaa benchi, kwani awali amekuwa havai hata jezi.
Ulimwengu tangu
asajiliwe Mazembe msimu uliopita, hii ni mechi yake ya kwanza anakaa benchi
kwenye michunao ya Afrika, hizi zikiwa ni dalili njema kwamba anakaribia kuanza
kucheza.
Katika mchezo huo,
kikosi cha Zamalek kilikuwa; Abdel Wahed El Sayed, Mahmoud Fathalla, A. Mendomo,
Sabri Rahil, Hazem Emam/ Said Kotta dk 77, Hani Saied, Ahmed Samir, Ibrahim
Salah/ Mohamed Ibrahim Islam Awad/dk63, R. Omotoyossi/ Ahmed Gaafar dk71.
Mazembe; M. Kidiaba, H.
Himoonde, F. Kasonde/ M. Ndonga dk 46
, J. Kasusula, S.
Sunzu, J. Kimwaki, R. Kalaba, P. Ochan/ N. Kasongo dk 63, M. Mputu, G.
Singuluma, M. Samata/ D. Kanda
Dk 86.
No comments:
Post a Comment