Tuesday, August 7, 2012

SIMBA NA CHUI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MWAKA HUU


CHAMA  cha Wakulima na Wafugaji kwa kanda ya kaskazini(TASO) kimesema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa na mabadiliko makubwa hasa kwa upande wa Ufugaji ambapo ndani ya maonesho hayo pia kutakuwa na maonesho ya wanyama mbalimbali kama vile Simba na Chui huku lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha zaidi kilimo kwanza hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw Athur Kitonga wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini hapa kuhusiana na maonesho ya wakulima na wafugaji kwa mwaka huu (Nane nane).

Bw Kitonga alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa ni maonesho ya tofauti na miaka mingine kwa kuwa kwa sasa wamewapa vipaumbele zaidi wafugaji na wakulima katika maonesho hayo tofaiuti na Miaka mingine ambayo kuna kuwa na wafanyabiashara wengi zaidi kuliko waoneshaji


Pia alisema kuwa ndani ya maonesho hayo ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza rasmi kuanzia kesho mpaka Agust 10 mwaka huu  kutakuwa na wanayama mbalimbali kama Vile Simba na Chui kutoka Jijini Dar es saalam ambapo napo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa ufugaji unakuwa ni wa kisasa zaidi

No comments:

Post a Comment