Kisukari (jina la
kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya
glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini
mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.
Dalili za
kisukari ni
- kukojoa kupitia kiasi cha kawaida
- kiuu kikubwa
- kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
- kuchoka haraka
- vidonda vinavyopoa polepole mno hasa kwenye miguu hadi kupotea viungo
UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini,ya mda
mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo
kinachoitwa insulin. Insulin hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya
kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji insulin ili kuweza kutumia sukari
tuliyonayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na
hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari ikizidi, ya ziada
inahifadhiwa katika ini kama mafuta. Mafuta haya hubadilishwa kuwa sukari na
kutumika wakati tukiwa na njaa kwa mda mrefu. Endapo kuna matatizo ya
kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na
inamaanisha ugonjwa wa kisukari upon a dalili kuanza kuonekana.
Viashiria vya ugonjwa wa kisukari (risk factors)
- Unene uliozidi na kiribatumbo
- Ulaji mbaya wa chakula
- Baadhi ya madawa
- Msongo wa mawazo
- Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
- Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
- Kutofanya mazoezi
- Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
- Magonjwa yanayoharibu kongosho
- Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
- Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
- Utumiaji uliozidia pombe na uvutaji sigara
Dalili za ugonjwa wa kisukari
·
Kiu ya mara kwa mara
·
Kupungua uzito licha ya kula
vizuri
·
Njaa kali na ya mara kwa mara
·
Jasho jingi
·
Uchovu usioeleweka hata bila
kufanya kazi
·
Kizunguzungu
·
Macho kupungua uwezo wa
kuona
·
Kidonda kisichopona haraka
Tiba ya ugonjwa wa kisukari
- Tiba bila dawa- ukigundulika unatakiwa kula chakula utakachoshauriwa na kufanya mazoezi ili ili kushusha sukari yako iwe ya kawaida.
- Tiba kwa vidonge-wengine hawawezi kutumia chakula tu kwa kushusha sukari hivyo wanapewa dawa za vidonge ili kushusha sukari yao pamoja na chakula.
- Tiba kwa kutumia sindano ya insulin-wanopata kisukari kabla ya miaka 35 lazima watumie insulin ili kuishi. Pia wagonjwa wa umri zaidi ya miaka 35 inawezekane sukari yao isishuke kwa vidonge hivyo namna ya tiba yao inabaki kuwa sindano tu.
Madhara ya ugonjwa wa kisukari
Endapo ugonjwa wa kisukari utapuuzwa au kutotibiwa
inavyostahili madhara mengi yanaweza kujitokeza na yanatokana na kiwango cha
sukari kuwa juu mwilini.
- Magonjwa ya moyo
- Kiharusi
- Kupungua nguvu za kiume
- Figo kushindwa kufanya kazi
- upofu
Ni matumaini
yangu wewe msomaji umenufaika na hili somo na pia utanufaishaisha familia na
jamii iliokuzunguka.
Kama hujapata huu ugonjwa ni muhimu kuepuka unene uliozidi
kwa kula lishe nzuri na ya kiasi, epuka pombe, msongo wa mawazo, pombe na
uvutaji wa sigara na la muhimu zaidi ni mazoezi ya viungo .
Tunashauriwa kupima kama tuna ugonjwa wa kisukari kila
mwaka, hivyo basi nenda mapema ili kuepuka madhara.
No comments:
Post a Comment