Didie Kavumbagu wa Yanga (Kushoto),ibu
kumtoka mlinzi wa African Lyon, kwenyepambano la soka ligi kuu ya
Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam yanga
imeshinda bao tatu kwa moja 3-1leo mabao yamefungwa na Nadir harub
kanavalo bao moja na Nizaa Khalfan amefunga mabao 2
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva,
(Kulia), akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Afrikan Lyon, Sunday
Bakari katika pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa
taifa jijini Dar es Salaam yanga imeshinda bao 3-1 leo
YANGA
imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Shukrani kwake
kiungo anayecheza kwa nadra kwenye timu hiyo, Nizar Khalfan aliyefunga mabao ya
ushindi dakika ya 65 na 88, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Nizar alifunga
bao la pili, sekunde chache baada ya Benedictor Mwamlangala kuisawazishia African
Lyon bao lililodumu tangu dakika ya 17, baada ya Nahodha wa Yanga, kutangulia
kufunga dakika ya 17.
Ushindi huo,
unaifanya Yanga ifikishe pointi saba, baada ya kucheza mechi nne na kupanda
hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa inalingana na Coastal kwa pointi
na wastani wa mabao, ingawa Coastal wako nyuma kwa mechi moja.
Simba bado
inaongoza ligi hiyo, kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10.
Yanga SC;
Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite,
Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi
'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo/Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu,
Hamisi
Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.
No comments:
Post a Comment