Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya “Daka Salio” iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel , pichani kushoto ni Afisa uhusiano wa Airtel na kulia ni Meneja bidhaa wa Airtel Salim Madati
Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akifafanua kuhusu huduma ya mpya ya “Daka Salio” wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Morocco na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akifuatiwa na Meneja Bidhaa Salim…
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya “Daka Salio” iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel , pichani kushoto ni Afisa uhusiano wa Airtel na kulia ni Meneja bidhaa wa Airtel Salim Madati
Maafisa wa Airtel kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya “Daka Salio” wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Morocco na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, kutoka kushoto ni Afisa mawasiliano na matukio Bi Dangio Kaniki, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando na Meneja Bidhaa Salim Madati.
AIRTEL YAJA NA KOPA NA UDAKE SALIO
- Salio la mkopo kutumika kupiga mitandao yote nchini
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa
kuendeleza dhamira yao ya Uhuru wa kuongea imetoa fulsa nyingine kwa
wateja wake kwa kuzindua huduma kabambe ya Daka salio ikiwa ni jitihada
zake katika kutimiza dhamira yake ya kuendelea kutoa uhuru wa kuongea
kwa wateja wake nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja
uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando by Jackson Mmbando alisema “Airtel
tumeamua kuleta huduma hii ya Daka salio kwa wateja wetu wote waendelee
kufurahia huduma zetu kila wakati, ikiwa sasa unaweza kukopa na kuongea
na ndugu au rafiki wa mtandao wowote sasa hakunakubeep tena.
Hii ni huduma nzuri kwa familia, marafiki
ndugu au jamaa kwa kuwa itaondoa tatizo la watu kubeep, Airtel tunasema
kwanini ubeep au uteseke kukopa kiwango kikubwa na kulipa zaidi. Daka
salio kidogo na ulipie kidogo na airtel. Ili kufurahia huduma hii ni
rahisi na haraka tuma tu neno daka kwenda 15549. Uongee mwanzo mwisho,
kwa raha zako.
Mteja yeyote anaweza kukopa ikiwa tu
amekuwa mteja wa Airtel kwa mfululizosiku tisini, awe anasalio la hadi
shilingi 50 na asiwe anadaiwa deni la Daka salio ikiwa alishakopa
kupitia huduma hii Faida ya kukopa salio ya Airtel ni kwamba
tunakukopesha kiwango kidogo ambacho utalipia kiduchu tu na utaongea kwa
muda mrefu. Achana na wanaokopesha kiwango kikubwa halafu unaongea
kidogo.
Mteja wa Airtel anaekopa salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na akitaka kulipa atalipa ziada ya sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu, kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500 bado utabakia na salio la kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel.
Mteja wa Airtel anaekopa salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na akitaka kulipa atalipa ziada ya sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu, kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500 bado utabakia na salio la kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel.
Airtel imekuwa na ubunifu wa bidhaa na
huduma zake zaidi kwa lengo la kufaidisha jamii kwa ujumla. Hivi
karibuni ilizindua huduma ya SUPA 5 yenye dili tano bomba na inaendelea
kutoa unafuu kwa wateja wa Airtel kupata sms 200 bure, kuongea na watu
watatu kwa nusu shilingi siku nzima, kupata huduma ya facebook bure ,
intaneti bure usiku, pamoja na kongea kwa robo shilingi nyakati za usiku
kwa kupiga tu *149*99# na kufuata utaratibu.
Airtel pia kupitia huduma yake ya Airtel
money inawawezesha wajasiliamali waliowekeza katika kwa kuwa wakala wake
nchi nzima pamoja na wateja wake, kwa wateja sasa wanapata mara mbili
ya salio wanaloongeza kupitia huduma ya Airtel Moneywakati WAKALA wote
nchi nzima watapata mara mbili ya kamisheni zao kwa mwezi juni - julai
kwa mihamala yote watakayofanya kupitia Airtel Money.
No comments:
Post a Comment