Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji (ambayo katika uamuzi
huu itarejewa kama ‘Kamati’) iliyokutana Julai 17 mwaka huu, baada ya
kupitia mikataba na nyaraka zote zinazohusiana na mchezaji Kevin Yondani
katika kujiridhisha juu ya hadhi yake ya usajili katika mashindano ya
Kombe la Kagame kama zilivyowasilishwa mbele yake imefikia uamuzi
ufuatao;
1. Kwa mujibu wa mapitio ya nyaraka zote zilizotajwa hapo
juu na kufanyiwa upembuzi yakinifu, Kamati iliridhika pasi na shaka
yoyote kuwa suala zima la mchezaji Kevin Yondani ni la kiutendaji, hivyo
uamuzi wa Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na Klabu ya Simba kwa suala
hilo la kiutendaji kama Sekretarieti ilivyofanya katika barua yake ya
Julai 14 mwaka huu ulikuwa sahihi.
2. Kamati ilibaini kuwa
Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba ulimalizika Mei 31
mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji Kevin Yondani kuanzia
Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.
3. Aidha Kamati
ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF ukiwa na
maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji Kevin Yondani
na Klabu ya Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu ambapo ni kinyume
cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji unaozitaka klabu
kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya wachezaji wao
wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba huo kwa jicho
la kisheria haupo.
4. Hata kama kamati ingeuona mkataba huo
katika jicho la sheria, bado mkataba huo una tatizo la kisheria hasa
katika tarehe ambazo pande mbili husika ziliingia makubaliano hayo.
Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa, wakati mchezaji Kevin Yondani
aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka jana, upande wa pili wa kimkataba
ambao ni Klabu ya Simba inaonekana iliingia makubaliano hayo kupitia kwa
Makamu Mwenyekiti wake Geofrey Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.
5.
Kisheria utata huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa
kurekebisha dosari hiyo kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko
hayo ili kuthibitisha mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria
mkataba huo hauwezi kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu
anayoipenda wakati akiwa huru.
Kutokana na maelezo yote hapo juu,
Kamati imeridhia hatua iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya
kumruhusu mchezaji Kevin Yondani kuichezea timu ya Yanga katika
mashindano ya Kombe la Kagame 2012
good day, to all the fantastic guys in Doha . i am new in Escorts in Doha and just arrived from Indian . i'm an Asian splendor with lovely exceptional appears, and slim and slim frame, and remarkable, sexy boobs and Lips. Doha Escorts prepared for all your offerings at my place in Heights or at your resort for a comfy night collectively. i am geared up for all forms of oral services and i am exceedingly experienced on this.
ReplyDelete