SINGIDA, TANZANIA
Mtu
mmoja amekufa baada ya kupigwa kufuatia vurugu kubwa zilizotokea kwenye
mkutano wa Chadema eneo la Iguguno mkoani, Singida. Imeripoti TBC 1
usiku huu.
Mwandishi wa kituo
hicho, aliyeko Singida, Leonard Manga amesema mrtu aliyeuawa alikimbizwa
na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa Chadema ambaoa walimfuata hadi katika
nyumba alimokimbilia ambako walimpiga hadi kumuua.
Amesema chanzo ni furugu zilizotokea kwenye mkutano wa Chadema
uliofanyika eneo la Iguguno, ambazo kwa mujibu wa mtangazaji huyo
zilisababishwa na Chadema kutoa maneno ya kumkashifu mbunge Mwigulu
Nchemba, jambo ambalo anadai lilisababisha watu waliopinga matusi hayo
walivurumisha mawe kwenye mkutano huo na kusababisha tafrani.
"Nadhani wale waliorusha mawe watakuwa ni wana-CCM ambao inaonekana
walichukizwa sana na maneno yaa kashfa yaliyokuwa yakitolewa na Chadema
kwenye mkutano huo dhidi ya Nchemba", alisema Mtangazaji wa TBC 1
Aliongeza; " wakati watu wakikimbia huku na huko naaba ya vurugu
kuwashinda polisi , mtu mmoja alikimbilia kwenye nyumba moja lakini
Chadema waliokuwa wanamkimbiza walimfuata na kumpiga hadi kumuua papo
hapo".
Amesema, kufuatia tukio hilo watu kadhaa wamekamatwa lakini haijathibitishwa kama ndiyo wanaohusika hasa na vurugu hizo.
No comments:
Post a Comment