Na Prince Akbar
MICHUANO
mipya ya soka ya BancABC Super 8, ambayo bingwa wake atazawadiwa Sh.
Milioni 40 na mshindi wa pili Milioni 20, inatarajiwa kuanza leo katika
miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha. Pia timu mbili
zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15
wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu
nane zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za
Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za
Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa
Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi
za ufunguzi leo ni kati ya Simba na Jamhuri Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Zimamoto na Mtende Uwanja wa Kirumba Mwanza, Mtibwa Sugar na
Polisi Morogoro Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha na Super Falcon na
Azam, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Awali
mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4, mwaka huu lakini yamesogezwa mbele
kwa siku moja na sasa hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu.
Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.
Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini
bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja
hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na
nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne
kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment