Timothy Bradley, Manny Pacquiao
Manny Pacquiao usiku wa kuamkia jana amepoteza taji lake kwa mara ya
kwanza baada ya kushindwa na Mmarekani, Timothy Bradley kufuatia uwamuzi
wa kutatanisha mjini wa majaji Las Vegas.
Licha ya Pacquiao bingwa huyo wa zamani kupiga ngumi 94 ikiwa ni
zaidi ya mpinzani wake, Mfilipino huyo alishindwa kwa mara ya kwanza
katika kipindi cha miaka saba baada ya majaji wawili kumpa Timothy
Bradley pointi 115-113.Watazamaji wa pambano hilo hawakuridhika na uamuzi uliotangazwa na walizomea sana baada ya Bradley kutangazwa mshindi kupelekea kuzua uwezekano wa pambano la marudiano baadaye mwaka huu.
“Nilihisi nimeshinda,” alisema Bradley, ambaye hapo kabla alikuwa amechapisha tiketi kabambe za kuonyesha pambano la marudano kufanyika Novemba 10, mwaka huu.
Bradley aliongezea; “Sidhani ni hodari kama wengi walivyomsifu. Makonde yake hayakua na nguvu.”
Pacquiao alichelewa kuingia ukumbini, lakini alipoingia alianza raundi ya kwanza kiuzembe uzembe ingawa alirusha ngumi tatu katika sekundi za mwisho wa raundi.
Hadi kufikia raundi ya tano, Bradley alionekana kuzidiwa kutokana na maumivu ya jeraha la kidole cha mguu, ikionekana kuwa Pacquiao anaelekea kupata ushindi wa mteremko.
Kwa upande wa Bradley alifanya vizuri katika raundi tatu za mwisho, lakini watazamaji hawakuridhika na hilo.
Pacquiao mwenyewe alisema hakuweza kuamini matokeo hayo. Aliongezea kuwa; “Nimejitahidi, lakini naona juhudi zangu hazikutosha. Ngumi zake hazikunidhuru, mara nyingi ngumi zake ziliishia kwenye mikono yangu,” alisema Pacquiao
No comments:
Post a Comment