KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Friday, August 3, 2012

UJUE UGONJWA WA KISUKARI,DALILI ZAKE,MADHARA NA TIBA MBADALA


Kisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.
Dalili za kisukari ni
  • kukojoa kupitia kiasi cha kawaida
  • kiuu kikubwa
  • kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
  • kuchoka haraka
  • vidonda vinavyopoa polepole mno hasa kwenye miguu hadi kupotea viungo
Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Watu walio wengi wana ushaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja mafuta mengi katika chakula na vyinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana

UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini,ya mda mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulin. Insulin hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji insulin ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari ikizidi, ya ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta. Mafuta haya hubadilishwa kuwa sukari na kutumika wakati tukiwa na njaa kwa mda mrefu. Endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari upon a dalili kuanza kuonekana.
 
Viashiria vya ugonjwa wa kisukari (risk factors) 
  • Unene uliozidi na kiribatumbo
  • Ulaji mbaya wa chakula
  • Baadhi ya madawa
  • Msongo wa mawazo
  • Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
  • Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
  • Kutofanya mazoezi
  • Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
  • Magonjwa yanayoharibu kongosho
  • Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
  • Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
  • Utumiaji uliozidia pombe na uvutaji sigara
Dalili za ugonjwa wa kisukari
·             Kiu ya mara kwa mara
·             Kupungua uzito licha ya kula vizuri
·             Njaa kali na ya mara kwa mara
·             Jasho jingi
·              Uchovu usioeleweka hata bila kufanya kazi
·             Kizunguzungu
·              Macho kupungua uwezo wa kuona
·              Kidonda kisichopona haraka
Tiba ya ugonjwa wa kisukari
  • Tiba bila dawa- ukigundulika unatakiwa kula chakula utakachoshauriwa na kufanya mazoezi ili ili kushusha sukari yako iwe ya kawaida.
  • Tiba kwa vidonge-wengine hawawezi kutumia chakula tu kwa kushusha sukari hivyo wanapewa dawa za vidonge ili kushusha sukari yao pamoja na chakula.
  • Tiba kwa kutumia sindano ya insulin-wanopata kisukari kabla ya miaka 35 lazima watumie insulin ili kuishi. Pia wagonjwa wa umri zaidi ya miaka 35 inawezekane sukari yao isishuke kwa vidonge hivyo namna ya tiba yao inabaki kuwa sindano tu.
Madhara ya ugonjwa wa kisukari
Endapo ugonjwa wa kisukari utapuuzwa au kutotibiwa inavyostahili madhara mengi yanaweza kujitokeza na yanatokana na kiwango cha sukari kuwa  juu mwilini.
  • Magonjwa ya moyo
  • Kiharusi
  • Kupungua nguvu za kiume
  • Figo kushindwa kufanya kazi
  • upofu
Ni matumaini yangu wewe msomaji umenufaika na hili somo na pia utanufaishaisha familia na jamii iliokuzunguka.
Kama hujapata huu ugonjwa ni muhimu kuepuka unene uliozidi kwa kula lishe nzuri na  ya kiasi, epuka pombe, msongo wa mawazo, pombe na uvutaji wa sigara na la muhimu zaidi ni mazoezi ya viungo .
Tunashauriwa kupima kama tuna ugonjwa wa kisukari kila mwaka, hivyo basi nenda mapema ili kuepuka madhara.

No comments:

Post a Comment