KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Sunday, August 5, 2012

BANC ABC SUPER 8 YAANZA LEO

 

Na Prince Akbar
MICHUANO mipya ya soka ya BancABC Super 8, ambayo bingwa wake atazawadiwa Sh. Milioni 40 na mshindi wa pili Milioni 20, inatarajiwa kuanza leo katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha. Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu nane zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi za ufunguzi leo ni kati ya Simba na Jamhuri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Zimamoto na Mtende Uwanja wa Kirumba Mwanza, Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha na Super Falcon na Azam, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4, mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja na sasa hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment