CHAMA cha Wakulima na
Wafugaji kwa kanda ya kaskazini(TASO) kimesema kuwa maonesho ya mwaka huu
yatakuwa na mabadiliko makubwa hasa kwa upande wa Ufugaji ambapo ndani ya
maonesho hayo pia kutakuwa na maonesho ya wanyama mbalimbali kama vile Simba na
Chui huku lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha zaidi kilimo kwanza hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw Athur Kitonga
wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini hapa kuhusiana na maonesho
ya wakulima na wafugaji kwa mwaka huu (Nane nane).
Bw Kitonga alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa ni
maonesho ya tofauti na miaka mingine kwa kuwa kwa sasa wamewapa vipaumbele
zaidi wafugaji na wakulima katika maonesho hayo tofaiuti na Miaka mingine
ambayo kuna kuwa na wafanyabiashara wengi zaidi kuliko waoneshaji
Pia alisema kuwa ndani ya maonesho hayo ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza rasmi kuanzia kesho mpaka Agust 10 mwaka huu kutakuwa na wanayama mbalimbali kama Vile Simba na Chui kutoka Jijini Dar es saalam ambapo napo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa ufugaji unakuwa ni wa kisasa zaidi
No comments:
Post a Comment