Juma Kaseja mazoezini
Bocco kulia na Poulsen
Kocha wa makipa Juma Pondamali kulia, akiwaongoza makipa Kaseja, Dida na Mwadini
Ngassa na Nyoni
Bahanuzi na Boban kulia
John BOKo na Boban
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imeanza maandalizi
ya mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana utakaochezwa Jumatano
ijayo mjini Gaborone.
Mdau wa blog alitembelea viwanja wa Karume jioni ya leo, na kuwakuta
wachezaji wa timu hiyo wakijifua chini ya walimu wao, Mdenmark Kim Poulsen na
wasaidizi wake Sylvester Marsh na Juma Pondamali.
Wachezaji waliokuwapo mazoezini ni makipa Deogratias Munishi
(Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha
msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo
(Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi
(Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon
Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC).
Stars inataria kuondoa jijini Dar es salam jumanne wiki ijayo tayari kwa pambano lao dhidi ya Botwsana.
No comments:
Post a Comment