KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Thursday, August 2, 2012

CHUJI AREJESHWA STARS, BAHANUZI NDANI, BARTHEZ AACHWA AITWA KIPA WA BENCHI

 
Na Prince Akbar

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen leo ametaja kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu, ndani yake akiwaita kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na mfungaji bora wa Klabu Bingwa ya Soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Hata hivyo, ajabu Poulsen amemuacha kikosini kipa Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ aliyedaka kwa umahiri mkubwa, mechi tatu za Kagame, Robo Fainali, Nusu Fainali na Fainali, hadi kuiwezesha Yanga kutwaa taji, huku akimuita kipa Mwadini Ally wa Azam, ambaye hajadaka hata mechi moja kwenye mashindano hayo.
Wachezaji wote walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samatta (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

No comments:

Post a Comment