MCHEZAJI
mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa rasmi jezi No,16
iliyokuwa ikitumiwa na mchezaji Mohamed Banka, ambaye pia alijiunga na
timu hiyo akitokea Yanga kabla ya kutemwa katika msimu uliopita.
Ngasa
sasa atakuwa akitumia jezi hiyo katika mechi za klabu yake mpya ya
Simza msimu huu, wa ligi Kuu unaotarajia kunza hivi karibuni.
Amesema,
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa
Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey
Nyange Kaburu.
Kaburu
alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi
wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake
mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu.
Tumeingia
naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka
Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani
yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan
Cirkovic, alikwa akiwahitaji sana" alisema.
Akizungumza
katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani
ni sawa na historia ya baba yake mzazi inajirudia, ambapo alikumbushia
kuwa hata baba yake mzazi, Khlfan Ngassa, aliwahi kuichezea klabu ya
Simba miaka ya 1990.
Kabla
ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na
wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es
Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre
Richard na James Kisaka.
No comments:
Post a Comment