KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Thursday, August 2, 2012

SURE BOY, AZAM WAMALIZANA SALAMA

 
                                                  Sure Boy arudi kazini
 

Na Prince Akbar
SALUM Abubakar ‘Sure Boy’ amemalizana salama na uongozi wa Azam FC, ambao umejiridhisha mchezaji huyo hakuhusika kwa namna yoyote kuihujumu timu hiyo katika fainali ya Klabu  Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya Yanga, Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Chanzo cha habari kutoka Azam kimesema kwamba, baada ya mazungumzo marefu kati yake (Sure Boy) na wamiliki, imekubalika mtoto huyo wa winga wa zamani wa Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ alisukumiwa ‘Jumba bovu tu’.
“Sure alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotoroka kambini usiku wa siku ya kuamkia mechi na Yanga, lakini alikuwa hajui chochote. Na hakuhusika, ila ameomba radhi na amesamehewa na hivi ninavyokuambia yupo hapa mazoezini,”kilisema chanzo chetu leo.
Azam wanaendelea na mazoezi chini ya makocha wake wa muda, Vivek Nagul kutoka India na Muingereza Kali Ongala, baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Stewart Hall kufukuzwa kazi juzi.
Stewart amefukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na kufunga bao la ushindi na kumuelezea kama mchezaji muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa ni asipangwe tena.
Katika fainali, Stewart alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho wa mchezo ikashinda 2-1 yeye akifunga la pili, dhidi ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwa kurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na Yanga ikashinda 2-0

No comments:

Post a Comment