KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Thursday, July 19, 2012

Mustakabali wa Van Persie kuamuliwa ndani ya saa 48 zijazo

Mustakabali wa Van Persie kuamuliwa ndani ya saa 48 zijazo
Klabu ya soka ya Arsenal ya Uingereza imeweka wazi kuwa suala la mshambuliaji wao nyota Robbin Van Persie litaamuliwa na  kuwekwa wazi ndani ya saa 48 zijazo. Gazeti la Daily mail la nchini humo linadai kuwa klabu ya Arsenal imemtaka mshambuliaji huyo kutoa tamko lake ndani ya saa 48 kabla ya kocha wa timu hiyo Arsene Wenger kuongea na vyombo vya habari juu ya hatma ya mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo ya washika bunduki wa London. Vyanzo vya ndani vya klabu hiyo vinadai kuwa Van Persie anatarajia kufanya mazungumzo na kocha wake kati ya Jumatano(leo) au Alhamisi ili kuweka wazi azma yake ya kuendelea au kutoendelea na mkataba mpya ndani ya klabu hiyo, Arsenal inatarajia kuanza tour yake katika bara la Asia siku ya jumamosi kwa ajili ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi. Hapo awali Arsenal walikuwa na nia ya kumjumuisha Van Persie kwenye tour hiyo lakini imethibika kuwa kama Van Persie ataweka wazi kuwa hakuna nafasi ya yeye kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo basi mshambuliaji huyo hataongozana na wenzake kwenye tour hiyo.

No comments:

Post a Comment