KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Tuesday, July 10, 2012

Dr.ASHA ROSE MIGIRO ALIVYOWASILI NYUMBANI TANZANIA


Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu
 Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati
 akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
 nchini Hoyce Temu.
 
Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
 pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
 
Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za
 Nje Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
 
Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga ardhi ya
 Tanzania.
 
Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa
 ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
 
Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na
 Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini 
Dr. Alberic Kacou.
 
Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
 baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.
 Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
 
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na
 Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika
 kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa JuliusNyerere.
 
Pichani Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday 
Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa
 aliporejea nyumbani.
  
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
 
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama.
 Akizungumza kwenye Iwanja wa Ndege, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
    Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa

No comments:

Post a Comment