KARIBU KATIKA BLOG HII YA KIJAMII



dstv

blog

Thursday, July 19, 2012

kufuatia ajali ya meli zanzibar, vodacom yaahirisha hafla ya kutoa tuzo maalum kwa mabloga bora


Baadhi ya wadau wa masuala ya blog nchini wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya jana katika hafla fupi iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kuwatunukia tuzo maalum, zoezi ambalo limeahirishwa kutokana na ajali ya meli iliyotokea mapema leo visiwani Zanzibar. Msemaji wa Vodacom amesema imebidi waahirishe zoezi hili ili kuungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa na kwamba kampuni hiyo ya simu itajiunga katika juhudi zozote za kujitolea kwa hali na mali katika maombolezo na kuwafariji waliopatwa na maafa pamoja na wafiwa.

No comments:

Post a Comment